Thursday, June 1, 2023

UWE NA MOYO WA UJASIRI

 UWE NA MOYO WA UJASIRI


Moyo wa ujasiri ni moyo uliojaa imani thabiti, ni moyo usiokata tamaa,  naam ni moyo usiyoyumbishwa na changamoto zinazotokea katika maisha, moyo huo ndiyo yatupasa tuwe nao ili tuweze kushinda katika safari yetu hapa duniani.


kila wakati jifunze kuwa na moyo wa ujasiri kwenye kila kitu unachofanya au unachotaka kufanya ili kuzifikia ndoto zako, usihofu kuhusu changamoto zinazojitokeza au zitakazojitokeza katika eneo ulilopo kwa sasa.


Elewa kwamba kila changamoto na ugumu ambao unakutana nao leo unasababu kubwa sana kama utatuliza akili yako na kutafakari juu ya ugumu huo. Haupaswi kukataa tamaa kwa sababu ya changamoto zinazojitokeza. 


Mara nyingi ugumu wa jambo fulani huwa una fumbo, ni vyema ukaelewa kwamba changamoto hazipo kukuangamiza bali zipo kukuimarisha kiimani na kisha uende viwango vingine.


 Kila hali ngumu unayokutana nayo leo ili hali hiyo uweze kuishinda yakupasa ujivika imani ya ujasiri kwa kumtegemea Mungu, wenda ni katika kazi, biashara, mahusiano n.k.


Epuka hali ya kukataa tamaa kwa sababu kila jambo lina ugumu wake hakuna jambo ambalo linapatiakana kiurahisi kama uzaniavyo, maana nyuma ya changamoto unazozipitia kuna mafanikio makubwa sana.


Nakusihi sana Rafiki yangu uwe JASIRI pale ukutanapo na hali ya ugumu katika kila jambo ufanyalo kwa kumshirikisha Mungu kila hatua upigayo, katu usirudi nyuma bali songa mbele.


Tambua wewe ni shujaa hivyo usikatishwe tamaa na changamoto mbalimbali unazokumbana nazo huwapo katika harakati za kuyafanikisha maono yako.


Neno la Mungu linatuhasa tuwe majasiri na hodari katika maisha, linasema:-


"...Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako." (Yoshua 1:9)


Moyo wa ujasiri unapatikana kwa kutambua ya kuwa Mungu yu pamoja nawe katika kila ufanyalo na katika kila mahali uendako, hivyo usiogope chochote kile mpendwa, wewe chapa kazi kwa bidii huku ukimtegemea Mungu na kila kitu kitakuwa sawa tu.


MUHIMU: "Usiombe maombi ya kuyafanya maisha yawe rahisi kwako, bali omba maombi ya kupata ujasiri na uhodari (uimara), maana uimara utakupa nguvu za kushinda kwenye huohuo ugumu uliopo kwenye maisha."


Kwa Mafundisho zaidi tembelea ukurasa huu ๐Ÿ‘‡๐Ÿฟ

https://biashara-news.blogspot.com?m=1

Pia nakuomba SHARE ujumbe huu kwa wengine nao wajifunze pia.


Nakutakia siku njema.

0 comments:

Ad