Saturday, June 3, 2023

NJIA ZITAKAZOKUSAIDIA KUPATA WAZO BORA LA BIASHARA / UJASIRIAMALI

 PART 1

njia zitakazokusaidia kupata wazo bora la biashara/ujasiliamali

Fursa na mawazo mbalimbali ya biashara yanatoka katika mazingira yanayotuzunguka; majumbani, makazini, mashuleni, safarini n.k Wajasiriamali waliofanikiwa hupata mawazo ya kuanzisha biashara, kuwa makini na kulifanyia kazi wazo la biashara alilolivumbua katika mazingira yanayomzunguka.


zifuatazo ni njia mbali mbali zitakazokusaidia kupata wazo la biashara/ujasiliamali


1.Kitu ukipendacho sana (hobby)

Mara nyingi watu hupenda kutumia muda fulani katika siku ama wiki kujiburudisha na vitu wavipendavyo mathalani kuchezea kompyuta, kupika, muziki, safari, michezo, na kufanya mazoezi.

Kutokana na kufanya jambo unalolipenda unaweza kuibua wazo la biashara, mathalani kuna watu wanapenda kunywa vilevi na mwisho wa siku wananzisha biashara ya baa.


2.Toka nje, jichanganye na watu

Ni vema ukatoka nje kujichanganya na watu ili uone fursa mbalimbali zilizopo kwa muda huo ambazo zitaweza kukusaidia ukatoa maamuzi ya kuanzisha biashara yako huku ukikutana na wafanyabiashara waliotangulia kwa kuiga tabia za kisiriamali.Mawazo ya kibiashara hayapatikani kwa kukaa ndani na kusubiri wazo lishuke kutoka mbinguni. Unahitajika ubunifu ambao unaweza kuupata kupitia maonyesho ya biashara, kutembelea wafanyabiashara wazoefu na kubadilishana mawazo. Ikiwezekana “wawinde” wafanyabiashara unaowafahamu ambao unaweza kuongea kuhusu wazo lako. Ishi kwa kuangalia wanavyoendesha biashara zao. Wengi hukatisha watu tama, usiwajali.


3.Maonyesho

Maonyesho ya kibiashara ni sehemu muhimu sana inayokutanisha wagavi, watengenezaji wa bidhaa mbalimbali, wanunuzi na wasambazaji. Kuhudhuria maonyesho ya biashara ambayo mara nyingi yanatangazwa kwenye vyombo vya habari itakusaidia kujifunza mengi kutoka kwa watu wengine na kuvutiwa na biashara ambayo unaweza kuifanya.


4.Malalamiko ya wateja

Tumia malalamiko ya wateja kama njia ya kupata wazo la kuanzisha biashara mpya. Mara nyingi tumekuwa tukishuhudia foleni kubwa kwenye benki, kucheleweshewa mkopo, magari ya abiria kujaza sana na vikwazo vingine vingi, katika hili pia unaweza kupunguza malalamiko hayo kwa kuanzisha biashara mpya.


Somolitaendelea

sharenamwenzakoajifunzepia

0 comments:

Ad