Saturday, June 3, 2023

NJIA ZA KUPATA MTAJI WA BIASHARA

 PART 1

NJIA ZA KUPATA MTAJI WA BIASHARA

Baada ya kuamua kuingia kwenye biashara/ ujasiriamali, sasa unahitaji mtaji wakufanyia na kukuzia biashara yako.

Mambo muhimu kuyajua:Sio kila biashara inahitaji mtaji au mtaji mkubwa! Kuna biashara zingine unahitaji tu kufahamiana na watoa bidhaa au huduma basi. Mfano biashara ya bodaboda, unahitaji tu kufahamiana na mwenye boda boda wewe unafanya kazi kwanza halafu unapeleka sehemu ya makubaliano yako na tajiri baadaye

Hata kama biashara yako itahitaji mtaji mkubwa unaweza siku zote funja funja hayo malengo ya biashara katika ngazi ambayo unaweza anza na mtaji unaoweza kumudu kuupata.Mfano unaweza kuwa unataka kuwa na hoteli kubwa ya biashara. Hapa unaweza anza na mgahawa na baadaye ikakua Mfano wa pili Labda unataka kuwa na supermarket, unaweza anza na mtaji wa 10,000 kuunza vitunguu, chumvi kwa nyumba za jirani mpaka ufukishe mwaka utakuwa na mtaji mkubwa ajabu.


Kama biashara yako itahitaji mtaji kwanza fikiria mambo manne (4) yafuatayo

1. Aina ya biashara (Kuzalisha, kuchuuza, huduma)

2. Aina ya soko (kipato kidogo, wanawake tu, wanaume tu, watoto tu, vijana tu, kijiji au mtaa tu nk)

3. Ukubwa wa mtaji (Mdogo, wa kati au mkubwa?)

4. Ufahamu wako kwenye biashara yako – Elimu/Ujuzi nk

Majibu ya maswali hapo juu ndio itakayoamua wewe upate mtaji wapi


Sasa swali, wapi utapata huo mtaji

1. Mali Binafsi

Kama una shamba, fedha, nyumba, gari, mifugo, mazao nk unaweza kutumia mali hizi kama mtaji wa biashara

Kumb. Ukishakubali kuwa mfanyabiashara wewe utakuwa daima ni mtu wa kununua na kuuza. Kwa hiyo hata kitanda chako unachokipenda sana kwa wakati fulani unaweza lazimika ukiuze ili upate mtaji wa biashara. Muhimu usiingie kichwa kichwa kwenye biashara na kujiletea hasara.


Faida ya aina hii ya mtaji#Haina riba, hata ikitokea bahati biashara ikafilisika haiwezi filisi na mali zingine kwani hakuna dhamana ya mali yako.


Hasara:# Hakuna msukumo wa biashara kwani mhusika hajali hata akipata hasara, Hivyo ni vigumu kupata faida na biashara kukua.


2. Wabia wa Biashara

Saa nyingine unatakiwa kuwatumia watu wengine ili kupata yafuatayo

1. Mtaji wa mali

2. Mtaji wa mawazo na fikra tofauti

Wabia wa baishara yako inaweza ongeza kasi ya kukua kwa biashara kwani fikra tofauti inaweza kuwa chachu ya maendeleo ya biashara husika ukiachilia mbali mtaji ambao wabia wako watakuja nao.

Inabidi lakini uwachague kwa uangalifu mkubwa wabia wako kwani wengine wanaweza kuwa ni wavurugaji na sio wa kuaminiwa.


Faida: Kuongezeka kwa kasi ya kukua kwa biashara kwa sababu ya fikra tofauti


Hasara: Mifarakano yenye kuweza kuua biashara ni dhahiri


3. Wawekezaji wa Biashara

Wawekezaji ni watu ambao wanaweza toa mali na pesa zao kukuwezesha wewe kufanya biashara yako lakini wao watahitaji baada ya muda wa uwekezaji warudishiwe pesa au mali zao na riba mliokubaliana kwenye mktaba wa uwekezaji.


Faida: Uhakika wa mtaji na hivyo uhakika wa kufanya biashara


Hasara: Biashara isipotengeneza faida kwa muda mliokubaliana inaweza sababisha kushitakiana na hatimaye biashara na mali zako kufilisiwa


4. Mkopo Kutoka kwa Watu wa Karibu

Ndugu/jamaa/marafiki na majirani wanaweza kuwa ni chanzo kizuri ya mtaji usio nariba.

Wanaweza kukupa fedha taslimu, wanyama, vitu kama mashine, mitambo, nyumba, ardhi, gari, kompyuta, na vifaa mbalimbali


Faida: Ni rahisi kupata mkopo bila mlolongo wa masharti, uwezekano wa kufilisiwa ni mdogo au hakuna kabisa


Hasara: Kwa vile ni mkopo wa ndugu/jamaa, jirani na marafiki, hakuna msukumo wa kufanya biashara kwa sababu hakuna kufilisiwa hivyo ni ngumu kupata faida na pia kukua kwa biashara yako


#SOMOLITAENDELEA

#SHARENAMWENZAKOAJIFUNZEPIA

0 comments:

Ad