Saturday, June 3, 2023

NJIA ZA KUPATA MTAJI WA BIASHARA

 PART 2

somo lililopita tulijifunza njia nne za kupata mtaji wa biashara pamoja na faida na hasara za kila njia. Sasa tunaendelea na njia zingine za kupata mtaji wa biashara


5. Mkopo Kutoka Kwenye Vyama, Vikundi nk

Vyama vya kijamii, kitaaluma, vikundi vya kuweka na kukopa, Vikoba vinaweza kuwa chanzo cha karibu kupata mkopo wa biashara wenye riba na masharti nafuu. Unachotakiwa tu ni kuwa mwanachama wa chama chenye kukopesha na kufuata masharti ya chama husika.


Faida: Uhakika wa mtaji japo unaaza na mdogo, uanweza kuepuka kufilisiwa mali zako. Kunakuweo na msukumo kwa kiwango fulani ya kufanya biashara na hivyo uwezekano wa kupata faida na biashara yako kukua


Hasara: Mtaji ni mdogo pale unapooanza


6. Mkopo Kutoka Kwenye Mashirika ya fedha (Micro-Credit Enterprises)

Mashirika kama Pride Tanzania, Vision Tanzania (zamani ikiitwa SEDA), Finca, Faida nk ni hatua nzuri kwa biashara ndogo kwani nao kama ilivyo vikoba wanatoa mikopo midogo kwa masharti nafuu.


Faida: Mlolongo mdogo, dhamana ni rahisi, wanaelimisha


Hasara: Riba ni kubwa, biashara ikifeli utafilisiwa mali ulizoweka dhamana


7. Mkopo kutoka Benki na Tasisi kubwa za Fedha

Mkopo unaohusisha benki ni sharti iwe ni biashara kubwa na mhusika awe na uhakika na soko pamoja na mtaji kurudi.

Mabenki mengine wanatoa mikopo mikubwa na midogo kwa pamoja.


Faida: Uhakika wa kupata mkopo mkubwa, pia msukumo wa kufanya biashara ni mkubwa na hivyo uwezekano mkiubwa wa kutengeneza faida


Hasara: Mlolongo wa kuupata ni mrefu, Kwa bahati mbaya biashara ikifeli, unafilisiwa haraka mali uliyoweka dhamana


Masharti ya mkopo

Unapokwenda benki  au taasisi nyingine za kifedha kuomba mkopo lazima utakutana na masharti yafuatayo ili uweze kupata mkopo huo. 

– Dhamana kama vile nyumba, arthi, mazao, kikundi n.k.

– Mchanganuo wa biashara

– Biashara inayo endelea(<miaka 3)

– Kuwepo kwa ofisi kama ni mkopo mkubwa zaidi ya milioni 3

– Biashara iliyosajiliwa kam ni biashara kubwa

– Riba ya mkopo

– Kiasi cha mkopo na uwezo wa mkopo

– Muda wa kurudisha mkopo na riba

#MWISHOWASOMO #SHARENAMWENZAKOAJIFUNZEPIA

0 comments:

Ad