Monday, May 29, 2023

Andika hivi matangazo yako ya mtandaoni

 


 


Kuandika matangazo yanayouza bidhaa au huduma yako ni hitaji la kila mfanyabiashara anayefanya matangazo ya kulipia mtandaoni.

 

 

Lakini usichokijua ni kwamba tangazo haliwezi likauza bidhaa au huduma yako.

 

 

Kwasababu kazi ya tangazo sio kuuza bidhaa au huduma yako.

 

 

Kazi ya tangazo ni kukuletea wewe mtu mwenye sifa za kuwa mteja wako ili wewe sasa ndio umgeuze mtu huyo kuwa mteja wako.

 

 

Tangazo lako halina utofauti na chambo kwa mvuvi.

 

 

Kazi ya chambo ni kuvuta na kushawishi samaki ang’ate ndoano.

 

 

Baada ya hapo kazi ni kwako mvuvi umchukue samaki ukamkaange, umchome, umuuze au umfanye vyovyote vile utakavyo.

 

 

Kwahiyo hata tangazo linafanya kazi sawa na chambo.

 

 

Tangazo litamshawishi msomaji akutafute kwa ajili ya kupata bidhaa au huduma yako.

 

 

Mtu akishakutafuta tangazo linakuwa limemaliza kazi yake.

 

 

Kazi yako ni kufanya juu chini mtu huyu aliye kutafuta ananunua bidhaa yako.

 

 

Asiponunua kuna uwezekano wa mambo 2 kutokuwa sawa.

 

 

  1. Hujui mbinu za kumclose mtu kuwa mteja wako

 

  2. Umelenga watu ambao hawana sifa za kuwa wateja wako hivyo tangazo linakuletea watu ambao sio sahihi kwa bidhaa au huduma yako.

 

 

Tuseme unajua kuclose vizuri ila unafeli kwenye uandishi wa tangazo lenye ushawishi kwa msomaji na unashindwa kulenga watu sahihi ili tangazo lako lionekane na lisomwe na watu wenye uhitaji wa bidhaa yako.

 

 

Kama tatizo lako ni hilo nina mashaka na uelewa wako juu ya mteja wako.

 

 

Nina uhakika 75% utakakuwa hujui sifa za mteja wako.

 

 

Fikiria unaongea kiswahili mbele ya mzungu asiyejua hata neno moja la kiswahili.

 

 

Ataishia kukushangaa tu maana atakuwa haelewi unachozungumza ni nini.

 

 

Kwahiyo hatua ya kwanza ya uandishi wa tangazo lenye kumshawishi msomaji kukutafuta ni kumuelewa mteja wako nje ndani.

 

 

Ukimuelewa mteja wako nje ndani ni rahisi kuandika tangazo ambalo linazungumza kwa mlengwa moja kwa moja.

 

 

Na utakachokiandika kwenye tangazo lako sio kuhusu bidhaa yako kwasababu mteja hajali hata robo kuhusu bidhaa au huduma yako.

 

 

Anachojali ni kuhusu yeye na yeye peke yake.

 

 

Kwahiyo utakachokiandika kwenye tangazo lako ni mambo 3.

 

 

Jambo #1: Anachokihitaji mteja.

 

 

Kila mtu anahitaji lake. Hitaji lako sio lake. 

 

 

Nitakuwa na uhitaji wa bidhaa yako endapo utanionesha kwamba kupitia bidhaa au huduma yako nitapata ninachokihitaji.

 

 

Kwahiyo bidhaa au huduma yako ni daraja tu, sio kitu ninachokihitaji.

 

 

Ninachokihitaji ni kile ambacho bidhaa yako inaenda kunifanyia.

 

 

Ukizungumzia kitu hicho ninachokihitaji halafu mwishoni ukaonesha kitu hicho nitakipata kupitia bidhaa yako basi sina budi kukutafuta uniuzie bidhaa yako.

 

 

Lakini ukizungumzia bidhaa yako hata sikuelewi maana unazungumza lugha isiyo eleweka kwenye ubongo wangu.

 

 

Usijisahaulishe kwamba hujui ubongo wangu saa zote unawaza kuhusu vitu ninavyovihitaji na sio vitu ambavyo watu wengine wanahitaji.

 

 

Kwanini nijali kuhusu bidhaa yako bila kuona umuhimu wa hiyo bidhaa kwangu?

 

 

Moving on…

 

 

Jambo #2: Maisha ya mteja yatakuwaje baada ya kununua bidhaa au huduma yako.

 

 

Kabla mteja hajanunua bidhaa yako kuna kitu anakikosa, si ndio?

 

 

Basi muelezee maisha yake yatakuwa na mabadiliko gani baada ya kupata bidhaa yako.

 

 

Kama nikinunua bidhaa yako sipati ongezeko lolote kwenye maisha yangu, kwanini sasa ninunue bidhaa yako?

 

 

Ongezeko linaweza kuwa furaha, pesa, mwonekano mzuri n.k 

 

 

Nitanunua bidhaa yako endapo utanionesha kwamba baada ya kununua bidhaa yako nitaondokana na kitu fuluni na nitapata kitu fulani kizuri zaidi kwenye maisha yangu.

 

 

Tunaelewana mpaka hapo?

 

 

Vizuri. Tumalizie…

 

 

Jambo #3: Mteja atapataje hitaji lake kupitia bidhaa yako?

 

 

Baada ya kuelezea kwamba kupitia bidhaa au huduma yako mteja atapata hitaji lake na ukaelezea ni utofauti gani bidhaa yako itauleta kwenye maisha yake…

 

 

Sasa ni wakati wa kumpa mteja wito wa kukupigia simu apate bidhaa yako, au aje whatsapp apate bidhaa yako….

 

 

Haijalishi ni sehemu ipi. 

 

 

Point ni kwamba unampa mteja maelekezo ya jinsi gani ataipata bidhaa yako.

 

 

Boom.

 

 

Mpaka hapo una tangazo makini sana la kukuletea utitiri wa watu ambao wapo tayari kununua bidhaa au huduma yako.

 

 

Usijifanye kipofu kwamba huoni ambacho mimi nimemaliza kukifanya kwako?

 

 

Nina darasa ambalo linafundisha kuhusu matangazo ya kulipia Facebook na Instagram.https://biashara-news.blogspot.com?m=1

 

 

Nina imani ningeanza post hii kwa kuzungumzia kuhusu darasa hili usingesoma mpaka mwisho.

 

 

Lakini kwakua najua hitaji lako ni wateja wengi mtandaoni nimeanza kwa kukufundisha kitu ambacho kitakusaidia kupata wateja hao ambacho ni uandishi wa tangazo lenye ushawishi.

 

 

Baada ya hapo nakupatia wito sasa ambao ni…

 

 

Kama unataka kujifunza kiundani njoo darasani sasa

https://biashara-news.blogspot.com/2023/05/andika-hivi-matangazo-yako-ya-mtandaoni.html



0 comments:

Ad